Ronaldo amekubali yaishe kawapa Tsh Bilioni 49.7



Jina la staa wa soka wa Juventus licha ya kumaliza tetesi zake za usajili kwa kusaini na kujiunga na Juventus ya Italia rasmi Cristiano Ronaldo, leo July 20 2018 jina lake limerudi tena kwenye headlines kuhusiana na tuhuma zake za ukwepaji kodi nchini Hispania.
Leo radio ya Cadena Cope ya Hispania imeripoti kuwa Ronaldo amekubali yaishe na kulipa kodi ya pound milioni 12.1 ambazo ni zaidi ya Tsh Bilioni 35.8 lakini pia atalipa pound milioni 4.7 kama faini ambao ni zaidi ya Tsh blioni 13.9, hivyo Ronaldo atakuwa kalipa jumla ya Tsh bilioni 49.7 ili kuepuka kifungo cha miaka miwili.

 Cristiano Ronaldo anaepuka kifungo cha miaka miwili jela kutokana na sheria za nchini Hispania kwa watu waliokutwa na hatia ya makosa yasiokuwa ya jinai na kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili kushuka chini, wanaweza kuepuka adhabu ya kifungo jela kwa kulipa faini.

Inadaiwa kuwa moja kati ya sababu zilizomsukuma Ronaldo kufanya maamuzi ya kuhama Hispania na kwenda Italia kucheza Juventus ni pamoja na kesi hiyo ya ukwepaji kodi, kwani aliogopa kupelekwa mahakamani, pia Ronaldo anadaiwa kuwa atauza nyumba yake ya kifahari yenye thamani ya pound milioni 4.8 sambamba na kuondoa biashara zake Hispania.

Comments

Popular posts from this blog

Janga la Yanga si la Kitoto

Mwinyi aongoza maziko ya baba mkwe wa Kikwete

HII NI NEEMA KWA MRISHO MPOTO