Mwinyi aongoza maziko ya baba mkwe wa Kikwete

Picha
RAIS mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi ameongoza maelfu ya watu kumzika baba mkwe wa Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, Mzee Rashid Mkwachu.
Mzee Mkwachu ambaye ni baba mzazi wa Mama Salma Kikwete, alizikwa jana saa 09:45 alasiri katika makaburi ya Kisutu Dar es Salaam. Alifariki dunia juzi baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Maziko hayo pia yalihudhuriwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda, wabunge, viongozi wa sasa wa siasa na serikali pamoja na wastaafu.
Akizungumza kwa niaba ya familia, mjukuu wa marehemu ambaye pia ni Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete alisema Mzee Mkwachu alikuwa rafiki na mtu muhimu katika familia na kuwataka watu kuiga mfano wake huku wakiendelea kumuombea apumzike mahala pema.
Viongozi wengine wa kitaifa walioshiriki maziko hayo ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Mbowe; Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT- Wazalendo, Kabwe Zitto, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki.
Pia walikuwapo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba, aliyekuwa Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange, aliyekuwa Jaji Mkuu, Othman Chande, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula na wanamichezo, aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage na Tarimba Abbas.

Comments

Popular posts from this blog

Janga la Yanga si la Kitoto

HII NI NEEMA KWA MRISHO MPOTO