Posts

Maneno ya Idris baada ya Wema kutakiwa kulipa faini ya Milioni 2

Image
  Baada ya hukumu ya Wema Sepetu kutoka leo July 20,2018 na kuhukumiwa mwaka mmoja jela au kulipa faini ya shilling Milion 2 kutokana na kupatikana na hatia ya kutumia dawa za kulevya aina ya bangi , Mpenzi wa zamani wa Wema Idris Sultan  ameandika yafuatayo. Idris amesema kuwa atamsaidia kulipa faini hiyo ya Milion 2 aliyoamuriwa na mahakama ambapo m aneno hayo ameyasema kupitia ukurasa wake wa instagram baada ya ku-post nusu picha ya Wema Sepetu na kuandika “🍒 wa sultan hawakai mbali na Sultan kama vipi nitalipa 😒”

HII NI NEEMA KWA MRISHO MPOTO

Image
Mrisho mpoto atoa shukrani kwa wananchi Baada ya kitendo cha Wananchi Kumpatia sifa juu ya Kudumisha na kupendelea kuvaa mavazi ya kiafrika ambayo akimalizia kwa kusema Hii ni nema Kwangu na Kuwahaidi watanzania ya Kwamba atakau nao bega kwa bega katika kurinda maadili ya mavazi na kuwashauri wasanii wenzake wajijengee tamaduni ya kutumia mavazi ya kinyumbani katika kazi zao za kisanaa.

Maagizo 10 ya Waziri Kangi Lugola kwa IGP na wengine

Image
  July 21, 2018 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola Alizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu matamko na maagizo mbalimbali aliyoyatoa tangu aapishwe kushika nafasi hiyo na Rais Magufuli. Nakusogezea Maagizo 10 aliyoyatoa wakati anaongea na Waandishi wa Habari. “Nimemuagiza Mkurugenzi wa NIDA afike Ofisini kwangu Dodoma tarehe 25 akiwa na waliopewa tenda ya kuleta mtambo wa kutengeneza vitambulisho vya Taifa kuja kunieleza kwa nini mtambo huo haujaletwa au waje na pesa walizopewa”.

Ronaldo amekubali yaishe kawapa Tsh Bilioni 49.7

Image
Jina la staa wa soka wa Juventus licha ya kumaliza tetesi zake za usajili kwa kusaini na kujiunga na Juventus ya Italia rasmi Cristiano Ronaldo , leo July 20 2018 jina lake limerudi tena kwenye headlines kuhusiana na tuhuma zake za ukwepaji kodi nchini Hispania. Leo radio ya  Cadena Cope ya Hispania imeripoti kuwa Ronaldo amekubali yaishe na kulipa kodi ya pound milioni 12.1 ambazo ni zaidi ya Tsh Bilioni 35.8 lakini pia atalipa pound milioni 4.7 kama faini ambao ni zaidi ya Tsh blioni 13.9, hivyo Ronaldo atakuwa kalipa jumla ya Tsh bilioni 49.7 ili kuepuka kifungo cha miaka miwili.   Cristiano Ronaldo anaepuka kifungo cha miaka miwili jela kutokana na sheria za nchini Hispania kwa watu waliokutwa na hatia ya makosa yasiokuwa ya jinai na kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili kushuka chini, wanaweza kuepuka adhabu ya kifungo jela kwa kulipa faini. Inadaiwa kuwa moja kati ya sababu zilizomsukuma Ronaldo kufanya maamuzi ya kuhama Hispania na kwenda Italia kuch

18 Mbaroni wakijaribu Kuua Tabora

Image
WATU 18 wanashikiliwa na Polisi mkoani Tabora wakihusishwa na matukio matatu tofauti, likiwemo la kujaribu kuua wanawake wanne. Wenye tuhuma za kujaribu kuua wanawake wanne kwa kuchoma moto ni 16 huku wengine wawili kwa tuhuma za mauaji. Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa polisi mkoa, Emmanuel Jackson ilisema kuwa wananchi kwa kushirikiana na polisi wa wilaya ya Kaliua waliweza kuwaokoa na kifo wanawake wanne waliokuwa wamekamatwa na walinzi wa jadi zaidi ya 200. Kamanda Jackson alisema kuwa Julai 16 mwaka huu saa nne usiku katika msitu wa Hifadhi ya Isawima, kata ya Igwisi wilaya ya Kaliua kiongozi wa sungusungu aitwaye Ingese Irea akiwaongoza wenzake 200 kuwakamata wanawake wanne. Alitaja wanawake hao kuwa ni Velediana Paulo (70), Modesta Magazi (45), Joyce Elias Magazi (33) na Nyamizi Dotto (40) ambao walitaka kuuawa wakituhumiwa kuwa ni wachawi. Aliongeza kuwa watuhumiwa hao na wenzao ambao bado wanasakwa waliwakamata wanawake hao kisha

Mashtaka watakiwa kutekeleza maagizo ‘Mpemba wa Magufuli

Image
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa siku sita kwa upande wa mashitaka katika kesi ya kujihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo inayomkabili mfanyabiashara Yusuf Ali “Mpemba wa Magufuli” kutoa taarifa ya utekelezaji wa maagizo, likiwemo la Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP). Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alitoa amri hiyo jana baada ya Wakili wa Serikali, Elizabeth Mkunde kudai kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi umekamilika. Pia alidai kuwa wapo katika utekelezaji wa maelekezo waliyopewa na DPP. Wakili wa Utetezi, Nehemia Nkoko alidai kuwa ahadi za upande wa mashitaka katika kesi hiyo ni za kawaida, hivyo wanaomba kujua washitakiwa hao watasomewa lini maelezo ya mashahidi. Hata hivyo, Hakimu Simba alisema mpaka wiki ijayo wawe wameeleza kesi hiyo imefi kia wapi na kuahirisha kesi hiyo hadi Julai 24, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Julai 5, mwaka huu, upande wa mashitaka uliieleza mahakama kuwa wanalifa

Ufaransa Waafrika ni wawili tu

Image
  WAAFRIKA wengi wameungana na raia wa Ufaransa kushangilia ubingwa wa Kombe la Dunia walioupata timu ya taifa ya nchi hiyo Jumapili iliyopita. Ufaransa waliibuka mabingwa wapya baada ya kuwalaza Croatia mabao 4-2 kwenye mchezo wa fainali uliopigwa mjini Moscow, Urusi. Waafrika wengi wamekuwa na furaha baada ya Ufaransa kulichukua kombe hilo kutokana na timu hiyo kuwa na idadi kubwa ya wachezaji wenye asili ya Afrika. Kati ya wachezaji 23 waliounda kikosi cha timu hiyo kwenye michuano ya Kombe la Dunia, wachezaji 13 wana asili ya Afrika. Wachezaji hao ni Presnel Kimpembe, Samuel Umtiti, Paul Pogba, Thomas Lemar, Kylian Mbappe, Ousmane Dembéle, Corentin Tolisso, N’Golo Kante, Blaise Matuidi, Steven Nzonzi, Steve Mandanda, Djibril Sidibe na Benjamin Mendy. Licha ya wachezaji wote hao kuwa na asili ya Afrika lakini ni wawili tu ndio walioonja joto la bara hili nikimaanisha kuwa wamezaliwa huku, lakini waliobaki wote wamezaliwa Ufaransa na kukulia nchini humo. Wal