18 Mbaroni wakijaribu Kuua Tabora

Picha
WATU 18 wanashikiliwa na Polisi mkoani Tabora wakihusishwa na matukio matatu tofauti, likiwemo la kujaribu kuua wanawake wanne. Wenye tuhuma za kujaribu kuua wanawake wanne kwa kuchoma moto ni 16 huku wengine wawili kwa tuhuma za mauaji.
Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa polisi mkoa, Emmanuel Jackson ilisema kuwa wananchi kwa kushirikiana na polisi wa wilaya ya Kaliua waliweza kuwaokoa na kifo wanawake wanne waliokuwa wamekamatwa na walinzi wa jadi zaidi ya 200.
Kamanda Jackson alisema kuwa Julai 16 mwaka huu saa nne usiku katika msitu wa Hifadhi ya Isawima, kata ya Igwisi wilaya ya Kaliua kiongozi wa sungusungu aitwaye Ingese Irea akiwaongoza wenzake 200 kuwakamata wanawake wanne.
Alitaja wanawake hao kuwa ni Velediana Paulo (70), Modesta Magazi (45), Joyce Elias Magazi (33) na Nyamizi Dotto (40) ambao walitaka kuuawa wakituhumiwa kuwa ni wachawi.
Aliongeza kuwa watuhumiwa hao na wenzao ambao bado wanasakwa waliwakamata wanawake hao kisha walikusanya kuni na kuwasha moto kwa dhumuni la kuwachoma.
Kamanda Jackson alisema kuwa wakati watuhumiwa wakiendelea ili kufanikisha unyama huo taarifa kutoka kwa wananchi wema zilifi ka polisi ambao bila kukawia walifi ka eneo la tukio na kuwaokoa na kufanikiwa kuwakamata baadhi yao.
Matukio ya aina hii ambayo yameegemea kwenye imani za kishirikina yanaendelea kushamiri katika vijiji mbalimbali vya mkoa wa Tabora hasa ambako wanaishi jamii ya wafugaji wa kabila la Wasukuma na kuupa mkoa sifa mbaya.
Mwishoni mwa mwaka uliopita watu wengine 55 wakazi wa kata ya Loya wilaya ya Uyui mkoani hapa akiwemo Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho walikamatwa baada ya jaribio lao la kutaka kuua wanawake wanne kwa kuwachoma moto kwa imani hizo hizo kushindikana.
Watuhumiwa hao bado wanakabiliwa na kesi mahakamani wakituhumiwa kwa makosa manne ya kujaribu kuua ambayo waliyatenda Septemba 17/2017.

Comments

Popular posts from this blog

Janga la Yanga si la Kitoto

Mwinyi aongoza maziko ya baba mkwe wa Kikwete

HII NI NEEMA KWA MRISHO MPOTO